Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2019

UJUMBE WA TASIHILI (A VALEDICTORY MESSAGE) KWA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA (MUST)

UJUMBE WA TASIHILI (A VALEDICTORY MESSAGE) KWA CHUO KIKUU CHA     SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA (MUST)


Naanza kwa kuishukuru Mamlaka ya Uteuzi kwa kuniwezesha kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kuanzia 2014 mpaka 2018. Aidha nawapongeza, Mhe. Pius Msekwa na Mhe. Zakia Meghji, kwa uteuzi wao kuwa Mkuu wa Chuo, na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, mtawalia. Nawatakia kila la heri katika ulezi na usimamizi wa Chuo.
Pili, ingawa nauita ushauri, kwa kweli ni ujumbe wa shukrani kwa Mamlaka ya Uteuzi na maelezo mafupi kuhusu uzoefu mdogo nilioupata nikiwa Mkuu wa Chuo Mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST). Kwani nitawezaje kutoa ushauri kwa Mkuu wa Chuo ambaye muda wake mrefu wa utumishi wake kwa Umma amekuwa katika maendeleo ya elimu ya juu, akiwa Makamu Mkuu Mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa maana hiyo MUST itafaidika pia kutokana na uzoefu na utumishi wa muda mrefu katika ngazi za …